Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano kati ya Ulaya na Asia ya Kati ni kuachana na dawa za wadudu za kizamani

Makubaliano kati ya Ulaya na Asia ya Kati ni kuachana na dawa za wadudu za kizamani

Nchi 12 za Ulaya Mashariki, Caucasus na Asia ya Kati wataanza kushirikiana na Muungano wa Ulaya na shirika la chakula na kilimo FAO kudhibiti akiba kubwa ya dawa za kuulia wadudu za kizamani. Muafaka huo umezinduliwa Alhamisi kwenye makao makuu ya FAO Roma.

Inakadiriwa kwamba takribani tani 200,000 za dawa za kuulia wadudu za kizamani karibu nusu ya dawa zote duniani zinapatikana katika nchi 12 za muungano wa zamani wa Soviet. Dawa hizo zimehifadhiwa mahali pasipo salama na zinatoa tishio kwa afya ya binadamu na mazingira.

Katika miaka mine ijayo Muungano wa Ulaya na FAO watawekeza euro milioni 7 kuuzisaidia nchi hizo ambazo ni Armenia, Azerbaijan, Belarus, Georgia, Kazakhstan, Kyrgystan, Moldova, Urusi, Tajikistan, Turkmenistan, Ukraine na Uzubekistan ili kdhibiti dawa hizo na kupunguza hatari.