Skip to main content

UM na washirika wake wazitaka Israel na Palestina kufufua mazungumzo kati yao

UM na washirika wake wazitaka Israel na Palestina kufufua mazungumzo kati yao

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake kwenye shughuli ya kutafuta amani eneo la mashariki ya kati wamezitaka Israel na Palestina kujizuia na vitendo vinavyosababisha kutokuwepo kuaminiana kati yao na badala yake kulenga katika kurejea tena kwenye mazungumzo ya moja kwa moja.

Wakitoa taarifa yao baada ya mkutano ulioandaliwa mjini Washington pande nne zinazojumuisha Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ulaya, Urusi na Marekani ziliezea kutofurahishwa kwao na vitendo kati ya Israel na utawala wa Palestina. Hata hivyo pande hizo nne zilikaribisha hatua ya Israel na Palestina ya kutatua masuasla yenye utata kati yao yakiwemo ukusanyaji wa ushuru.