Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azitaka Sudan Kusin, Sudan kuchukua hatua za haraka kuepusha machafuko zaidi

Ban azitaka Sudan Kusin, Sudan kuchukua hatua za haraka kuepusha machafuko zaidi

Katika majadiliano yake na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa mwito wa kukomeshwa kwa machafuko yanayoendelea sasa baina ya taifa hilo la jirani yake Sudan.

Ban amesema kuwa viongozi wa pande zote wanapaswa kuchukua hatua za haraka kusitisha mapigano hayo kabla umwagikaji wa damu haujapindukia.

Katika majadiliano hayo kwa njia ya simu, Ban amemtaka rais wa Sudan Kusini Kiir kufiria hatua ya kuitisha mkutano wa marais kujadilia mkwamo huo na kufungua ukurasa wa majadiliano kutanzua hali hiyo ya sintofahamu.

Pande hizo mbili kwa wiki kadhaa sasa zimekuwa zikichafuana katika kile kinachoonekana ugombaniaji wa rasilimali muhumu zinazopatikana upande wa Sudan Kusini.