Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lazima liwajibike kwa pamoja kuikabili Korea Kaskazini-Marekani

Baraza la Usalama lazima liwajibike kwa pamoja kuikabili Korea Kaskazini-Marekani

Baraza la Usalama lazima lichukue hatua makini kukabili hali ya mambo iwapo taifa la Korea Kaskazini litazindua kituo cha kurusha makombora ya masafa marefu.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema kuwa Baraza la Usalama lazima likubaliane kuchukua hatua muafaka kukabili tabia ya Korea Kaskazini. Amesema kuwa iwapo taifa hilo litafikia hatua hiyo, itakuwa ni kuyaendea kinyume maazimio kadhaa ya Umoja wa Mataifa ambayo yanapiga marafuku kuanzisha luteka zozote za kijeshi.

Amesisitiza haja ya Baraza hilo la Usalama kuwa na maamuzi ya pamoja kukabili tabio yoyote kengeufu itayoonyeshwa Korea Kaskazini.