Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muigizaji wa kichina kuwa daraja baina ya wakimbizi wa Kisomali

Muigizaji wa kichina kuwa daraja baina ya wakimbizi wa Kisomali

Mcheza sinema wa Kichina Yao Chen amehitimisha ziara yake ya kwanza Afrika kama mwakilishi wa heshima wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi UNHCR kwa Uchina, ambako amepongeza ujasiri wa wakimbizi wa Kisomali na karibu wa Ethiopia inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi hao.

Yao Chen alikwenda Ethiopia wiki jana kukutana na wakimbizi wa Kisomali kwenye kambi za mpakani za Dollo Ado na Jijiga na kusema anahisi hali hiyo inahitaji kufuatiliwa kwa karibu kwani wakimbizi hao wanahitaji msaada sasa. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)