Syria yamhakikishia Annan kuwa itatekeleza mpango wa kusitisha mapigano

11 Aprili 2012

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria Kofi Annan amesema mmoja wa washirika wakubwa wa Damascus ambayo ni Iran inaweza kusaidia kutatua mzozo wa Syria. Annan yuko nchini Iran kujaribu kutafuta uungwaji mkono wa mpango wake wa kusitisha machafuko ya Syria kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hata hivyo Annan ameonya kwamba mipango yoyote mibovu nchini Syria inaweza kusababisha janga kubwa. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Annan amesema ni muhimuu sana kwa misaada ya kibinadamu kufika katika maeneo yaliyoathirika mara moja na kwamba pande zote lazima zishirikiane. Kwa kushindwa kutekelezwa kwa muda wa mwisho wa kusitisha mapigano hapo April 10 Annan amesema bado kuna matumaini ya kumalizika kwa machafuko lakini ameongeza kuwa hali inasalia kuwa tete.

(SAUTI YA KOFI ANNAN)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter