Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washiriki wajiandaa kuhudhuria mkutano wa Rio+20

Washiriki wajiandaa kuhudhuria mkutano wa Rio+20

Ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kundaliwa mkutano wa Rio+20 nchini Brazil waakilishi kutoka serikali kote duniani wanajiandaa kuhudhuria mkutano huo ambao utajadili maendeleo endelevu katika siku za baadaye. Kati ya masusla yanayotarajiwa kuzungumziwa kwenye mkutano huo ni kupunguzwa kwa hewa zinazochafua mazingira pamoja na uchumi usioathiri mazingira. Mfano ni ndege walio na makao yao nchini Mexico lakini wenye asili yao nchini Brazil ambao wamechangia kwa sehemu fulani katika kuboreka kwa sekta ya pamba nchini Marekani.

Wakati wa msimu wa joto ndege hao hufunga safari kutaga mayai hadi kati kati mwa Mexico na kusini maghaharibi mwa Marekani ambapo chakula chao huwa nai wadudu waharibifu. Kulingana na utafiti uliofanywa ni kwamba njia hizi za kiasili za kuungamiza wadudu waharibifu zina manufaa ya dola 740.000 kwa uchumi wa marekani.