Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Iraq ni lazima wafanye kazi pamoja ili kutatua masuala:Kobler

Viongozi wa Iraq ni lazima wafanye kazi pamoja ili kutatua masuala:Kobler

Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema hali ya kisiasa pamoja na uwezekano wa matatizo kutokana na vurugu nchini Syria ni masuala ambayo yanaendelea kutatiza nchi hiyo.

Martin Kobler ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo Jumanne kwamba Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq utaendelea kusaidia nchi hiyo mpaka itakaporudi katika hali ya kawaida.

Amesema ni muhimu kwa viongozi wa Iraq kufanya kazi pamoja ili kuondoa vikwazo vya kisiasa nchini humo na kwamba jukwaa la umoja ni muhimu katika kuhutubia tofauti zao.

"Kuendelea kwa ucheleweshaji wa kuitisha mkutano wa kitaifa kunasisitiza haja ya viongozi wa Iraq kutafuta haraka utashi wa kisiasa na ujasiri wa kufanya kazi pamoja ili kutatua matatizo ya nchi kupitia njia ya makubaliano.

Pia ameeleza wasiwasi kuhusu haki za binadamu nchini hasa katika suala la majeruhi wa kiraia, unyanyasaji wa kijinsia na hali ya watu wasio raia na waliokimbia makazi yao.