Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanadiplomasia wa UM alaani shambulizi la bomu kaskazini mwa Kosovo

Mwanadiplomasia wa UM alaani shambulizi la bomu kaskazini mwa Kosovo

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo, amelaani vikali tukio la shambulizi la bomu lilitokea mwishoni mwa wiki katika majengo kadhaa yaliyoko kaskazini mwa mji wa Mitrovica.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa, bomu hilo liliwekwa kwenye dirisha la jengo moja na baadaye kulipuka na kuuwa mtu mmoja na wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Akilaani tukio hilo mwanadiplomasia Farid Zarif ametaka mamlaka za dola kuchunguza mara moja na wahusika wake kufikishwa kwenye mkono wa dola.

Ametuma salama za rambirambi kwa ndugu na jamaa waliofikwa tukio hilo na ametaka wananchi wa eneo hilo kushikamana kwa pamoja kuyakabili maovu hayo.