Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyikazi wa kibinadamu na msaada umeimarika nchini Syria

Wafanyikazi wa kibinadamu na msaada umeimarika nchini Syria

Syria inaikubali Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu (ICRC) kuimarisha shughuli za kibinadamu nchini humo, kwa mujibu wa Shirika hilo.

ICRC inasema kwamba serikali ya Syria imekubali kusitisha vita ili kuyawezesha mashirika ya kibinadamu kuhamisha waliojeruhiwa..

Makubaliano hayo yaliafikiwa wakati wa ziara ya rais wa ICRC Jakob Kellenberger Damascus wiki jana.

Rabab Al-Rifai ni msemaji wa ICRC Damascus.

(SAUTI YA RABAB AL-RIFAI)

Chama cha msalaba mwekundu kina karibu watu 70 Syria ambao wamewasilisha msaada katika miji ilioathirika zaidi ikiwemo Homs, Idlib na Deraa.