Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani kuendelea kwa mashambulizi kwa raia Syria

Ban alaani kuendelea kwa mashambulizi kwa raia Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali kuzuka tena kwa mashambulizi dhidi ya raia nchini Syria, mashambulizi ambayo yanajiri katika wakati ambapo serikali ya Assad iliahidi kuviondosha vikosi vyake kwenye maeneo ya raia. 

Ban ameutaka utawala wa Assad kutembea kwenye maneno yake kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kukukomesha mashambulizi kwa raia na kuvirejesha kambini vikosi hivyo. 

Katika taarifa yake, Ban amelaani dhidi ya matumizi ya nguvu ya kijeshi kuwaandama raia wasiokua na hatia akisema kuwa kitendo cha namna hiyo hakiwezi kukubalika kwenye macho ya dunia. 

Hapo siku ya jumatatu, serikali ya Syria ilimwarifu mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Nchi za Kiarabu Kofi Annan  kwamba itakamilisha kuondosha vikosi vyake ifikapo April 10.