Skip to main content

UM wataka kuheshimishwa kwa haki za binadamu inapoendelea oparesheni ya ukusanyaji silaha

UM wataka kuheshimishwa kwa haki za binadamu inapoendelea oparesheni ya ukusanyaji silaha

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umewataka wanajeshi wa nchi hiyo kuhakikisha kuwa haki za binadamu zimeheshimiwa wakati kunapondelea oparesheni ya kukusanya silaha kwenye jimbo la Jonglei.

UNMISS inasema kuwa hata kama shughuli hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa njia ya amani na utulivu kumekuwa na ripoti  za ukiukaji wa haki za binadamu kwenye sehemu kadha.

Kati ya ukiukaji wa haki za binadamu ulioripotiwa ni pamoja na kupigwa na kuhangaishwa kwa raia wakati vikosi vya usalama vilipoendesha oparesheni ya nyumba hadi nyumba.