Gharama kubwa na huduma duni ni tatizo kwa afya ya jamii

7 Aprili 2012

Leo ni siku ya afya duniani, Umoja wa Mataifa waungana na dunia kuadhimisha siku hii ambayo kwa mwaka huu inajikita kupiga darubini masuala ya afya na uzee.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa na afya njema ni chachu ya watu kuishi maisha bora na marefu kwa faina ya familia na jamii zao.

Hata hivyo imekuwa ni mtihani mkubwa kwa watu hasa kutoka nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo umri wa watu kuishi unakadiriwa kutozidi miaka 50.

Na tatizo hasa nihuduma dunia za afya, ambapo nyingi ziko mijini na zikipatikana gharama yake ni kubwa kwa wengi kumudu.

Wananchi hawa wanasema endapo serikali hazitofunga kibwebwe na kusaidia watu wake wasiojiweza kupata huduma hizo watu wengi watapoteza maisha na kufikia uzeeni itakuwa ni kitendawili.

(MAONI BURUNDI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter