Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha siku ya afya duniani kwa kuangalia changamoto zinazowakabili wazee

UM waadhimisha siku ya afya duniani kwa kuangalia changamoto zinazowakabili wazee

Pamoja na kwamba maandalizi ya sikukuu ya pasaka yanaendelea vilevile dunia na Umoja wa Mataifa kwa ujumla wanajiandaa kuadhimisha siku ya afya duniani ambayo kila mwaka hufanyika April 07.

Kauli mbiu ya siku ya afya mwaka huu inahusiana na masuala ya uzee na afya, na mada za siku hiyo zitajikita katika kuangalia ni jinsi gani tabia zinazozingatia masharti ya afya katika maisha zinaweza kuwasaidia wanawake na wanaume wazee kuishi maisha kamilifu na na marefu zaidi yanavyoweza kuwa rasilimali muhimu katika familia na jamii zao.

Matatizo ya kiafya ni mengi na mara nyinmgi waathirika wakubwa hwa ni wanawake na watoto.

Leo mwandishi wetu wa Dar es salaam Tanzania George Njogopa anaagazia matatizo makubwa mawili ya kiafya yanayosumbua wanawake, ambayo ni saratani na fistula. Ungana naye.

(MAKALA GEORGE NJOGOPA)