Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UM yafahamishwa kuhusu hatma ya wafungwa wa kipalestina nchini Isreal

Kamati ya UM yafahamishwa kuhusu hatma ya wafungwa wa kipalestina nchini Isreal

Mkuu wa kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wapalestina anasema  kuwa amepokea habari  kuhusu hali ya wafungwa wa kipalestina kwenye magereza ya Israel.

Mwenyekiti wa kamati ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa Palestikna Abdou Salam Diallo amesema kuwa sheria ya kimataifa ni lazima iheshimiwe akiongeza kuwa mashambulizi dhidi ya Israel ni lazima yakome.

Kwenye mkutano wa siku mbili uliondaliwa mjini Geneva masuala matatu muhimu yalizungumziwa yakiwemo kukamatwa na kuzuiliwa kwa wapalestina na hatma ya kisheria kwa wafungwa wa kipalestina.