Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zinaendelea kushuhudiwa kwenye miji ya kaskazini magharibi mwa Libya

Ghasia zinaendelea kushuhudiwa kwenye miji ya kaskazini magharibi mwa Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya unaelezea wasi wasi wake kutokana na kuendelea kwa ghasia kwenye miji mitatu iliyo kaskazini magharibi mwa nchi.

Ujumbe wa UNSMIL umezitaka pande zinazohusika kwenye mapigano kwenye miji ya Zuwara, al-Jumail na Regdalin kusitisha ghasia na kukubaliana na jitihada za utawala za viongozi za kuleta utulivu.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ian Martin amesema kuwa watu wa Libya walijitolea maishani yao wakitafuta taifa lenye demokrasia.

Mapigano ya hivi maajuzi kwenye mji wa Zuwara yanavuruga jitihada za utawala za kuhakikisha kuwepo idara za kiusalama zilizo dhabiti.