Skip to main content

UNRWA inaadhimisha siku ya afya duniani

UNRWA inaadhimisha siku ya afya duniani

Katika kuadhimisha siku ya afya duniani itakayokuwa hapo Jumapili Aprili 7, Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA inafanya shughuli mbalimbali Ukanda wa Gaza, Jordan, Lebanon, Syria na Ukingo wa Magharibi ili kuchagiza suala la kuzeeka na matatizo yanyowakabili wazee.

Shughuli watakazofanya zinaambatana na kauli mbiu ya siku ya afya duniani mwaka huu ambayo ni “afya njema inaongeza umri wa kuishi” shughuli hizo zitajumuisha upimaji damu na uelimishaji jamii kuhusu masuala ya uzee.

Mkurugenzi wa mpango wa afya wa UNRWA Fr Akihiro Seita anasema kauli mbiu ya mwaka huu ni muafaka kwa dunia na kwa wakimbizi milioni 5 wa Kipalestina .