Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika na Asia kuongoza katika ongezeko la watu mjini:UM

Afrika na Asia kuongoza katika ongezeko la watu mjini:UM

Bara la Afrika na Asia yataongoza katika ukuaji wa idadi ya watu mijini katika miongo mine ijayo, hali ambayo italeta changamoto mpya katika upatikanaji wa ajira mijini, masuala ya nyumba, nishati na miundombinu umesema Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa takwimu za matarajio ya ukuaji wa miji duniani kwa mwaka 2011 zilizotolewa Alhamisi na Umoja wa Mataifa zinasema idadi ya watu mijini barani Afrika itaongezeka kutoka milioni 414 na kupindukia bilioni 1.2 ifikapo mwaka 2050 huku barani Asia idadi ikipanda kutoka bilioni 1.9 na kufikia bilioni 3.3.

Mabara yote hayo mawili yatakuuwa na jumla ya ongezeko la asilimi 86 ya ongezeko lote duniani .

Takwimu hizo pia zinasema ongezweko hilo litatoa fursa mpya za kuboresha elimu na huduma za jamii Afrika na Asia kwa kuwa itakuwa rahisi kuwafikia watu walio wengi.

Hata hivyo hofu ni changamoto zitakazotokana na ongezeko hilo la watu umesema Umoja wa Mataifa hasa katika kupambana na umasikini, kupanuka kwa mitaa ya mabanda na kuharibika kwa mazingira mijini.