Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yaipongeza Brazil kutokana na kuwajibika kikamilivu kudhibiti majanga

UM yaipongeza Brazil kutokana na kuwajibika kikamilivu kudhibiti majanga

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema amesifu na kupongeza juhudi za Brazil kushiriki kwake kikamilifu kwenye maeneo ya utoaji misaada ya kiutu akisema kuwa nchi hiyo imetoa msaada mkubwa kwenye maeneo ya kukabiliana na majanga na usalama wa chakula.

Bi Valerie Amos amesema kuwa anatiwa moyo na kuvutiwa na namna nchi hiyo ilivyomstari wa mbele kuweka mipango yenye lengo la kukabiliana na majanga, malengo ambayo yametoa msaada mkubwa kwenye uso wa dunia.

Amesema Umoja wa Mataifa una azma ya kuendelea kushirikiana na taifa hilo kwenye eneo la kusaka njia bora za kukabili majanga ambayo yanakwamisha juhudi mbalimbali za ustawi jumla.

Bi Amos ameeleza hayo baaada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu nchini humo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika eneo la Latin Amerika.