Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sista wa DR Congo awasaidia wanawake walioathirika na ghasia za LRA:UNHCR

Sista wa DR Congo awasaidia wanawake walioathirika na ghasia za LRA:UNHCR

Sista Angelique anawasiadia wanawake DR CongoShirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema mtawa mmoja wa kikatoliki sista Angelique amekuwa akijitolea kuwasaidia mamia ya wanawake walioathirika na machafuko yanayofanywa na waasi wa Uganda wa LRA kwenye mji wa Dungu.

Sista huyo anazunguka na baiskeli kuwatembelea wanawake walioathirika na kutekwa, kubakwa na kujeruhiwa na waasi wa LRA.

Wanawake hao wanamuona sista Angeliquue kama Baraka baada ya kundi la LRA kuwaacha maelfu ya watu wakiishi na woga Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)