Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga alaani mashambulizi ya kujitoa mhanga nchini Somalia

Mahiga alaani mashambulizi ya kujitoa mhanga nchini Somalia

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga ameelezea hasira zake kutokana na shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea kwenye ukumbi wa Sanaa mjini Mogadishu nchini Somalia wakati kulipokua kukiendelea sherehe ambapo watu sita waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Akiongea kutoka mjini Istanbul ambapo alikuwa akikutana na maafisa kutoka Uturuki kutafuta uungwaji mkono kwenye masuala yalio njiani nchini Somalia, Mahiga alionyesha huruma yake kwa watu wa Somalia.

Mahiga ametoa wito kwa viongozi nchini Somalia na watu wa Somalia kutosahau mpango wa amani na uwiano.