Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sidibe aipongeza Algeria kutokana na jitihada zake za kupumbana na ugonjwa wa ukimwi

Sidibe aipongeza Algeria kutokana na jitihada zake za kupumbana na ugonjwa wa ukimwi

Michel Sidibe,UNAIDS na Waziri wa Afya,AlgeriaMkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS Michel Sidibe amelipongeza taifa la Algeria na kulitaja kuwa bingwa kwenye vita dhidi ya ukimwi.

Hatua za mapema za taifa la Algeria dhidhi ya ugonjwa wa ukimwi zimezaa matunda ambapo nchi hiyo imeandikisha maambukizi kidogo ya ugonjwa huo.

Tangu mwaka 1998 serikali ya Algeria imekuwa ikitoa bila malipo madawa yanayopunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi kwa wale wote wanaoyahitaji.

Pia maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa wa watoto ni tatizo ambalo limeangamizwa nchini Algeria.

(SAUTI YA GRACE KANEIYA)