Huu ni wakati muhimu wa kutekelezwa kwa haki za binadamu nchini Chad:KANG

4 Aprili 2012

Naibu kamishina kwenye tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Kyung wha-Kang amekamilisha ziara yake nchini Chad akisema kuwa wakati serikali ina kibarua kigumu katika kuboresha hali ya haki za binadamu nchini Chad siku za usoni, inaonekana wazi kuwa upande wa siasa uko tayari kufanya hivyo.

Bi Kang amesema kuwa uhaba wa chukula, dhuluma dhidi ya wanawake, ukwepaji wa sheria, kutokuwepo uhuru wa mahakama na kuwahamisha watu kwa nguvu kama baadhi ya masuala yanayohusiana na haki yanayoikabili nchi hiyo.

Akihutubia waandishi wa habari mjini N’Djamena alipokamilisha ziara yake Kang alisema kuwa huu ni wakati muhimu kwa suala la haki za binadamu nchini Chad.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud