Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti zaidi kuhusu virusi vya H1N1 wafanyika

Utafiti zaidi kuhusu virusi vya H1N1 wafanyika

Utafiti kuhusu virusi vya H1N1Utafiti zaidi kuhusu virusi vya H1N1 unaendelea kwenye nchi zenye  kipato cha chini na cha wastani tangu kutokea janga la ugonjwa huo mwaka 2009.

Hii ni kulingana na makala kutoka kwa shirika la afya duniani WHO ambapo wanasayansi nchini China wanasema kuwa ugonjwa wa H1N1 unasababisha vifo vingi zaidi  tofauti na ilivyochukuliwa nchini humo.

Pia kulingana na makala nyingine ni kwamba virusi vya  H1N1 huwa  vinasababisha kuugua kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwenye sehemu za vijiji magharibi mwa Kenya huku watafiti nchini Australia na Indonesia wakitafuta njia za kuzuia maambukizi ya virusi hivyo kwenye masoko ya wanyama.