Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DFID kwenye makubaliono ya dola milioni 25 na FAO

DFID kwenye makubaliono ya dola milioni 25 na FAO

Ufadhili utaboresha kilimoIdara inayohusika na maendeleo ya kimataifa nchini Uingereza DFID imetia sahihi  makubaliano na shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO wa kutoa dola milioni 25 kufadhili  uvumbuzi na ushirikiano mpya wa dunia ambao utaboresha takwimu za kilimo kwa serikali na wakulima kote duniani.

Jitihada za  kuboresha takwimu za kilimo inazisaidia nchi zinazoendelea katika kutoa  na kutumia takwimu za kilimo kwa usalama wa chakula na pia katika kuwasaidia wakulima kupata habari  wanapoihitaji. 

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)