Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubalino mapya ya kuzuia biashara haramu ya bidhaa za tumbaku yaafikiwa

Makubalino mapya ya kuzuia biashara haramu ya bidhaa za tumbaku yaafikiwa

Baada ya miaka minne ya majadiliano shirika la kimataifa linalohusika na majadiliano INB pamoja na mataifa 135 yaliyoshiriki wamekubaliana kupiga marufuku biashara haramu ya bidhaa za tumbaku.

Mwenyeki wa INB  Ian Walton Geroge amesema kuwa kwa kuafikia makubaliano hayo nchi zimeonyesha kujitolea kwao katika kulinda afya ya umma na kukabiliana na biashara haramu kwa bidhaa za tumbaku.

Makubaliano hayo yanatoa sheria za kupambana na biashara haramu ya bidhaa za tumbaku.

Chini ya makubaliano hayo wanachama walikubaliana kushirikiana katika kufuatilia bidhaa za tumbaku na kwenye masuala ya utoaji wa leseni.