Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR bado yatilia shaka idadi ya wakimbizi waliotokana na machafuko ya eneo la Balkans

UNHCR bado yatilia shaka idadi ya wakimbizi waliotokana na machafuko ya eneo la Balkans

Mnamo wakati ikipita miongo miwili sasa tangu kutokea kwa uharibifu wa kibinadamu wakati wa machafuko eneo la Balkans, shirika la Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi limeelezea hali mbaya inayowaandama wakimbizi wengi wanaondelea kusalia kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu wa UNHCR mamia ya watu waliyolazimika kukimbia makwao wakati wa machafuko hayo ya mwaka 1991 hadi 1995, walirejea kwenye maeneo yao ya asili na kufungamana na jamaa zao.

Lakini hata hivyo bado kunasalia kundi kubwa la wakimbizi ambao bado wameendelea kusalia kwenye maeneo ya mtawanyiko.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Melissa Fleming,kuna hali ya mkwamo inayoendelea kuwaandama idadi kubwa ya wakimbizi kutokana na machafuko hayo yaliyodumu kwa kipindi cha miaka minne na kusababisha zaidi ya watu 200,000 kupoteza maisha.