Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kwa viongozi wa Israel na Palestina kuanza tena mazungumzo ya moja kwa moja:Ban

Ni muhimu kwa viongozi wa Israel na Palestina kuanza tena mazungumzo ya moja kwa moja:Ban

Ni muhimu kwa viongozi wa Israel na Palestina kuanza tena mazungumzo ya moja kwa moja yakiwa na lengo la kufikia makubaliano ya kuwa na nchi mbili zinazoishi pamoja kwa amani.

Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja Ban Ki-moon katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Kimataifa juu ya Swali la Palestina, uliofanyika mjini Geneva Jumanne.

Katibu Mkuu Ban amesema kuwa vikwazo vimezuia tena Waisraeli na Wapalestina kuweza kuendelea na majadiliano.

Amesema mada mbalimbali ambazo zinahitaji kupewa kipaumbele haraka ni pamoja na hatma ya wafungwa Wapalestina walio kizuizini Israel. Martin Nesirky ni msemaji wa Katibu Mkuu.

(SAUTI YA MARTIN NESIRKY)

Ujumbe wa Katibu Mkuu ulisomwa kwenye mkutano wa Geneva na Maxwell Gayland, Naibu mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Mchakato wa Amani Mashariki ya Kati.