Ban ataka Sudan Kusini, Sudan kukomesha mapigano

3 Aprili 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kutoridhika kwake na namna mapigano yanavyoendelea kuchacha huko mpakani baina ya Sudan na Sudan Kusin na amezitaka pande zote kukutana mara moja kwa ajili ya kukomesha machafuko hayo.

Amezitolea mwito serikali zote mbili kutambua wajibu wa kukomesha machafuko hayo ambayo yameendelea kugharimu maisha ya raia.

Hadi sasa hali ya wasiwasi imezidi kuongezeka kufuatia ripoti za kuwepo kwa mapigano ambayo yanaweza kusababisha hali ya usalama kwa pande zote mbili kuwa mbaya zaidi.

Pande zote mbili zimekuwa kwenye majadiliano ya namna kuyakwamua masuala yaliyozua utata, hasa baada ya Sudan Kusin kuwa jamhuri hivi karibuni.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud