Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 20 tangu kutokea kwa machafuko yaliyokuwa Yugoslavia

Miaka 20 tangu kutokea kwa machafuko yaliyokuwa Yugoslavia

Wiki hii inatimia mwaka wa 20 tangu kutokea kwa mauwaji ya kutisha huko iliyokuwa zamani Yugoslavia, mauwaji ambayo yalisababisha watu zaidi ya 200,000 wakipoteza maisha na mamilioni wengine kuingia ukimbizoni.

Sokomoko hilo lililodumu kwa muda wa miaka minne, linatajwa kuleta maafa mabaya zaidi barani Ulaya ukiweka vita vya pili vya dunia.

Watu wengine wapatao 400,000 waliokuwa wakiishi mji mkuu wa Bosnia walikosa makazi na hivyo kuzusha kitisho kingine kikubwa cha kijamii.

Lakini hata hivyo, wakati kukiadhimishwa mwaka huo wa 20, wengi ya raia waliokwenda uhamisho kukimbia machafuko hayo yaliyodumu kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 wamerejea makwao na kuchangamana na jamaa zao.