Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ndiyo mwanzo wa maendeleo:Ban

Elimu ndiyo mwanzo wa maendeleo:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa elimu ndio mwanzo wa maendeleo. Akihutubia mkutano wa marais wa viuo viku mkwenye chuo kikuu cha Columbia Ban amesema kuwa kuna masuala matatu muhimu yakiwemo Elimu, ajira na kuwawezesha vijana.

Ban amesema kuwa kuna takriban vijana milioni 74 wasiokuwa na ajira duniani na kuwa vijana wanastahili kupata elimu na pia ajira. Ban ameongeza kuwa kwa kuwawezesha vijana pia inahitaji kuwepo ushirikiano nao na hili ndilo Umoja wa Mataifa unajaribu kufanya.