Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yataka kutolewa kwa msaada wa dharura nchini Syria

OCHA yataka kutolewa kwa msaada wa dharura nchini Syria

Takriban watu milioni moja wanahitaji huduma za kibinadamu nchini Syria. Hii ni kulingana na matokeo ya wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa na ushirikiano wa kiislamu walioshiriki kwenye uchunguzi uliondeshwa na serikali.

Shirika la kuratibu masuala ya kibindamu la Umoja wa Mataifa OCHA inasema kuwa idadi hiyo ni ya watu walioathirika moja kwa moja na ghasia. Habari kutoka kwa uchunguzi huo ina maana kuwa kwa sasa kuna picha nzuri kuhusu kile wanachohitaji kwa dharura ukiwemo msaada wa chakula na madawa, vyombo vya nyumbani na ushauri wa kisaikolojia na elimu.

OCHA inasema kuwa mashirika ya kibinadamu nchini Syria yatahitaji kuongeza huduma zake ili kuweza kutoa huduma za dharura.