Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji haramu wa watoto kwa minajili ya ajira waongezeka:IOM

Usafirishaji haramu wa watoto kwa minajili ya ajira waongezeka:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa idadi ya watoto wanaosafirishwa kiharamu na waliookolewa na IOM iliongezeka hadi watoto 2,040 mwaka 2011 ikiwa ni aslimia 27 zaidi kutoka watoto 1,565 mnwaka 2008. Takwimu mpya kutoka IOM inaonyesha kuwa idadi ya watu wazima wanaosafirihswa kiharamu ilipanda kwa asilimia 13 kutoka watu 3,012 hadi watu 3,404.

Usafirishaji haramu wa watu kwa lengo la ajira uliongezeka kwa asilimia 43 hadi watu 2,906 kutoka watu 2031 mwaka 2008. Visa vya usafirisha haramu wa kimataifa vilipingua kwa asilimia 13 hadi watu 3531 mwaka 2011 kutoka watu 4,006 mwaka 2008. Jumbe Omari Jumbe ni kutoka IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)