Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yana hofu hali ya watu nchini Mali

Mashirika ya UM yana hofu hali ya watu nchini Mali

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaelezea hofu iliyoko kuhusiana na hali ya kibindamu nchini Mali ambapo maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano na ukosefu wa chakula.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa usalama kwenye eneo la kaskazini mwa nchi unaendelea kuwa mbaya kutokana na kuibuka kwa makundi yaliyojihami.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa limelazimika kusitisha usambazaji wa chakula katika sehemu za kaskazini mwa Mali baada ya kuvamiwa na kuporwa kwa ofisi zake.

Zaidi ya watu 200,000 wamelazimika kuhama makwao kaskazini mwa Mali tangu mwezi Januari.

Melisa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa takriban wakimbizi 400 kutoka Mali huingia Burkina Faso na Mauritania kila siku.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)