Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya nzuri huchangia maisha marefu:WHO

Afya nzuri huchangia maisha marefu:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu walio na umri wa miaka 60 na zaidi inatarajiiwa kupanda na kuzidi idadi ya watoto walio chini ya miaka mitano kwa muda wa miaka mitano ijayo.

WHO kwa sasa inatoa wito wa kutaka kutolewa kwa huduma za kiafya kwa watu wazee na kuondoa vizuizi vinavyowazuia kushiriki vilivyo kwenye masuala ya kitaifa.

Changamoto kubwa kwa watu wazee ni magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, kiharusi, saratani, ugonjwa wa kisukari pamoja na magonjwa ya moyo.

Hata hivyo WHO inasema kuwa hatari ya kuugua magonjwa kama haya miaka ya uzeeni inaweza kupunguzwa kwa kusihi kwa njia iliyo bora kiafya na kukula vyakula bora na pia kuzuia matumizi ya pombe. Dr John Beard ni kutoka WHO.

(SAUTI YA DR.JOHN BEARD)