Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya usalimishaji silaha kwa hiari inapaswa kuendelezwa

Kazi ya usalimishaji silaha kwa hiari inapaswa kuendelezwa

Nassir Abdulaziz Al-NasserUkosefu wa dhamira ya kisiasa kunaathiri kazi ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa mashirika yanayohusika na maswala ya usalimishaji silaha kwa hiari, hii ni kwa mujibu wa Rais wa Baraza kuu. 

Wakati wa kufunguliwa rasmi kikao cha tume ya usalimishaji silaha kwa hiari (UNDC) mjini New York jumatatu Balozi Nassir Abduaziz Al-Nasser amesema kuwa mashirika ya usalimishaji silaha kwa hiari yamefika mahali muhimu sana kwani yanakumbwa na kile alielea kama upinzani unaoongezeka dhidi ya ari na maafikiano.

Anasema swala la UNDC na Kongamano la usalimishaji silaha kwa hiari, umesababisha kukwama kwa kazi ya pande zote mbli kwa zaidi ya muongo moja.

Hali hii haiwezi kuendelea na haipaswi kuendelea. Kwa kuzingatia hayo ameongeza kuwa hawezi himiza zaidi majukumu na fursa ambayo wao wote wako nayo leo ya kuweka utaratibu wa kurejesha kazi ya uwaslishaji silaha kwa hiari ikiwemo ya UNDC katika utaratibu unaofaa.