Kujiuzulu kwa jaji na mabadiliko mengine Cambodia kunatia mashaka:Ban

2 Aprili 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema matukio ya hivi karibuni kwenye mahakama ya Cambodia ikiwemo kujiuzulu kwa jaji wa kimataifa wa upelelezi Siegfried Blunk kumezusha hofu kuhusu mchakato mzima unaohusiana na kesi 003 na 004, na mazingira ya kujiuzulu kwa jaji bado yanatia mashaka.

Jaji Bknk anahusisha kujiuzulu kwake na kuingiliwa kwa kesi hizo mbili na serikali ya kifalme ya Cambodia. Baraza kuu la Cambodia halikumteua jaji Kasper-Ansermet kama mpelelezi mshiriki wa kimataifa kama ilivyotakiwa na makbaliano baina ya Umoja wa mataifa na Cambodia. Hata hivyo ameendelea kutimiza wajibu wake na kuhitimisha kwamba kumekuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za mahakama katika uchungzi wa kesi 003 na 004. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud