Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano kuchagiza uwekezaji katika sayani, teknolojia na ubunifu Afrika:UNESCO

Kongamano kuchagiza uwekezaji katika sayani, teknolojia na ubunifu Afrika:UNESCO

Kuisaidia Afrika kufikia mahitaji ya elimu ya juu katika masuala ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati ni moja ya malengo ya mkutano wa siku tatu unaoendelea mjini Nairobi Kenya.

Kongamano la kwanza la Afrika kuhusu sayansi, teknolojia na ubunifu kwa ajira ya vijana, maendeleo ya binadamu na maendeleo yanayojumuisha wote limeandaliwa na mashirika mbalimbali likiwemo la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

Kwa mujibu wa UNESCO kongamano hilo lililoanza Jumapili linatoa fursa za kubadilishana uzoefu pamoja na kuunda sera ambazo zitachagiza ubunifu, ujasiriliamali na ajira kwa wanawake na vijana. Lidia Brito ni afisa wa UNESCO.

(SAUTI YA LIDIA BRITO)

Washiriki 200 wanahudhuria kongamano hilo wakiwemo mawaziri wa sayansi na elimu, wawakilishi kutioka sekta za habari na mawasiliano, teknolojia, afya na fedha, pia wanafunzi na jumuiya za vijana