Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya FAO ina dhamira ya kujenga uwezo wa kuwafikia maskini

Ripoti ya FAO ina dhamira ya kujenga uwezo wa kuwafikia maskini

Kuongeza uzalishaji wa kilimo ni moja ya nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini, lakini uwekezaji katika kilimo na maendeleo vijijini unaweza usifikie malengo endapo utashindwa kutilia maanani mazingira ya kijamii yanayoathiri maisha na usalama wa chakula.

Hayo yamesemwa katika ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo FAO yenye lengo la kuchagiza uwekezaji kwa kusisitiza umuhimu wa miradi ambayo itakuwa na picha kamili ya kuwajumuisha wadau wote na kuzingatia usawa wa kijinsia. Grace Kaneiya anaripoti.

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)