Teknolojia ni muhimu katika kupunguza gesi ya Carbon siku za usoni

2 Aprili 2012

Broadband inaweza kusaidia kuihamishia dunia katika uchumi wa matumizi madogo ya cabon na kushughulikia chanzo na athari za mabadiliko ya hali ya hewa imesema ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu na tume ya broadband kwa ajili ya maendeleo ya digital.

Daraja la broadband kuunganisha teknolojia ya mawasiliano na hatua za hali ya hewa ni matokeo ya kazi iliofanywa na tume hiyo ya broadband kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

Ripoti hiyo ina lengo la kuuchagiza umuhimu na jukumu la teknolojia ya habari na mawasiliano ICT na hasa katika mitandao ya broadband ambayo inaweza kusaidia kujenga uchumi wa matumizi madogo ya cabon hapo baadaye na kuelezea umuhimu wa ushirikiano baina ya sekta za umma na binafsi katika kuharakisha mabadiliko hayo.

Kwa mujibu wa mkurgenzi wa ITU Hamadoun Toure kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa ni kubadili kabisa jinsi watu wanavyoishi, kufanya kazi, kusafiri, na jinsi ya kupiga hatua za maendeleo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud