Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazima mataa kwa saa moja kuonyesha uzalendo kwa wasio na umeme

UM wazima mataa kwa saa moja kuonyesha uzalendo kwa wasio na umeme

Umoja wa Mataifa  Jumamosi ulizima taa kwa muda wa saa moja kwenye makao yake makuu mjini New York na sehemu zingine kote duniani katika kile kinachofahamika kama “Saa ya Dunia” Suala ambalo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa hamasisho ya kutaka kuchukuliwa hatua za kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja wa Mataifa ulizima taa zake ili kuonyesha uzalendo kwa wanaume , wanawake na watoto ambao hadi sa hawajafikiwa na umeme. Huu ndio mwaka wa tatu Umoja wa Mataifa unaungana na mamilioni ya watu wengine duniani katika kuzima taa. Mwaka uliopita zaidi ya miji mikubwa 5200 na mingine midogo 135 ilishiriki kwenye shughuli hii.