Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ayataka mataifa kuunga mkono jitihada za kumaliza mzozo nchini Syria

Ban ayataka mataifa kuunga mkono jitihada za kumaliza mzozo nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezishauri nchi zilizohudhuria mkutano kuhusu Syria mjini Istanbul nchini Uturuki kuunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu katika kumaliza mzozo ulio kwenye taifa hilo la mashariki ya kati ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 8000 tangu mwezi Machi mwaka uliopita.

Ban amesema kuwa hatua kubwa zimepigwa tangu kuandaliwa kwa mkutano wa kwanza wa nchi marafiki ya Syria uliondaliwa terehe 24 mwezi Februari mjini Tunis huku nchi zikimuunga mkono mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu Kofi Annan.