Wataalamu wa chakula kukutana kutathmini hatua na changamoto Afrika

2 Aprili 2012

Zaidi ya wataalamu wa chakula 45, wabunge, taasisi za haki za binadamu na watunga sera kutoka Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Afrika ya Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe watakutana mjini Nairobi Kenya kuanzia Aprili 4 hadi 5 kujadili jinsi ya kuimarisha ulinzi wa chakula katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Mkutano huo umeitishwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya haki ya chakula Olivier De Schutter kwa msaada wa ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO.

Lengo la mkutano huo ni kujaribu kuksanya uzoefu na kujenga maarifa kuhusu mitazamo ya haki za binadamu katika kupambana na njaa katika kanda hiyo.

(RIPOTI YA JASON NYAKNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud