Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bunge bado ni muhimu katika masuala ya demokrasia:UNDP/IPU

Bunge bado ni muhimu katika masuala ya demokrasia:UNDP/IPU

Ripoti ya pamoja iliyotolewa Jumatatu na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na mungano wa mabunge IPU inasema bunge bado ni nguzo muhimu katika jitihada za umma kwa demokrasia licha ya uaminifu tete.

Ripoti inasema mabunge hii leo yanakabiliwa na uchunguzi wa umma na shinikizo kuliko ilivyokuwa zamani huku maswali yakijitokeza kuhusu uwezo wake wa kuiwajibisha serikali.

Hata hivyo ripoti imeongeza kuwa licha ya changamoto hiyo mabunge wakati huu ni muhimu sana katika maisha ya kisiasa ya nchi.

Hii ni ripoti ya kwanza ya kimataifa kuhusu bunge ambayo inaangalia mfumo wa mabadiliko katika uwakilishi wa bunge.

Ripoti inasema ili kushughulikia hali ya imani ndogo kwa bunge mabunge lazima yawashirikishe wananchi , yawe karibu na mahitaji yao na yafanye juhudi kukidhi matakwa ya wananchi.