Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bhutan inatambua umuhimu wa furaha kwa pato la taifa:Ban

Bhutan inatambua umuhimu wa furaha kwa pato la taifa:Ban

Serikali ya Bhutan imetambua umuhimu wa furaha ya taifa dhidi ya pato la nchi tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970 amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akizungumza Jumatatu kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu furaha na maisha bora katika kueleza dhana mpya ya uchumi, Ban amesema Bhutan imeridhia malengo ya kufikiwa furaha ya kitaifa dhidi ya uzalishaji wa taifa kwani masuala haya yanakwenda sambamba.

Mtazamo huo kwa mujibu wa Ban umeanza kuchagiza maeneo mengine kufuata mkumbo.

Ametoa mfano wa Costa Rica ambayo amesema ndio inayohifadhi mazingira kuliko sehemu yoyote duniani na imepiga hatua za maendeleo za kimazingira ukilinganisha na nchi zenye kipato kama chake na ni mfano wa kuigwa katika masuala ya amani na demokrasia.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)