Mradi mpya wazinduliwa kufikisha dawa bora na rahisi Afrika:UNAIDS

2 Aprili 2012

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS limesema haja ya kuhakikisha watu wa Afrika wana fursa ya kupata dawa muhimu  zenye ubora, salama na za gharama nafuu imepata msukumo mpya baada ya kuzinduliwa mradi wa Afrika ya Mashariki wa uandikishaji wa madawa mjini Arusha Tanzania hapo Machi 30.

Mradi huo ni muungano wa ngazi ya juu unaowaleta pamoja mshirika mpya kwa ajili ya maendeleo ya Afrika NEPAD, shirika la afya duniani WHO, wakifu wa Bill na Melinda Gates, Bankiya dunia, idara ya Uingereza ya maendeleo ya kimataifa na mradi wa fursa za afya wa Clinton CHAI.

Uzinduzi wa mradi huo Arusha unaashiria mwanzo katika utekelezaji wa mipango mingi ya udhibiti wa madawa barani Afrika.

Washirika katika mradi huo wanatumai kuimarisha uwezo wa udhibiti na mifumo kwa ajili ya madawa barani afrika ikiwa ni pamoja na dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV’s ili kuhakikisha maisha yanayopotea na maradhi ya ukimwi kutokana na dawa zisizo salama na za ubora usifaa yanapunguzwa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud