Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay kufanya ziara ya kwanza kabisa nchini Barbados

Pillay kufanya ziara ya kwanza kabisa nchini Barbados

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay atafanya ziara rasmi nchini Barbados kwa mwaliko wa serikali kuanzia tarehe 3 hadi 5 mwezi Aprili mwaka huu.

Ziara hii ndiyo itakuwa ya kwanza kufanywa na mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye taifa la Caribbean tangu kubuniwa kwa ofisi hiyo mwaka 1993.

Wakati wa ziara hiyo Pillay anakutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Freundel Stuart, mawaziri, maafisa wa ngazi za juu, pamoja na kiongozi wa upinzani.

Pia atafanya mashauriano na majaji akiwemo jaji mkuu na rais wa mahakama ya Caribbean na pia wanachama wa mashirika ya umma.