Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 100,000 wakimbia mapigano kaskazini magharibi mwa Pakistan

Zaidi ya watu 100,000 wakimbia mapigano kaskazini magharibi mwa Pakistan

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa usaidizi kwa maelfu ya familia nchini Pakistan ambazo zimekimbia mapigano kwenye sehemu kadhaa za makabila nchini humo  kwenye mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan.

Takriban watu 101,160 wengi wakiwa  wanawake na watoto wamelazimika kuhama tangu tarehe 20 mwezi Januari wakati vikosi vya serikali vilipoanzisha oparesheni za usalama dhidi ya makundi ya wanamgambo kwenye eneo la Khyber.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)