Skip to main content

Afisi ya haki za binadamu ya UM yahuzunishwa na kuuawa kwa msenge nchini Chile

Afisi ya haki za binadamu ya UM yahuzunishwa na kuuawa kwa msenge nchini Chile

Afisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea mshangao wake kutokana na kuuawa kwa mwanamme mmoja msenge nchini Chile.

Afisi hiyo sasa inatoa wito kwa serikali ya Chile kuweka sheria ambayo itapiga marufuku kutengwa kwa watu kuambatana na tabia zao za kimapenzi.

Washukiwa wanne wameshatiwa mabaroni huku mauaji hayo yakizua mjadala mkali  nchini Chile ambapo watu wengi walikesha nje ya hospitali  ambayo Zamudio alipelekwa baada ya kushambuliwa.

Tukio hilo linaonekana kuwa ghasia zilizochochewa na chuki dhidi ya  wasenge, mabasha na wanaobadili jinsia kote duniani.

Kulingana na ripoti iliyowasilishwa kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa  mapema mwezi huu ilionyesha kuongezaka kwa ghasia, dhuluma na mauaji dhidi ya  wasenge, mabasha na wale wanaobadili jinsia.