Ugonjwa wa Surua waua zaidi ya watoto 100 nchini Yemen

30 Machi 2012

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa mkurupuko wa ugonjwa wa surua umewaua watoto 177 nchini Yemen huku wengine 4000 wakiambukizwa ugonjwa huo  kwa muda wa miezi michache iliyopita.

UNICEF inasema kuwa kuzorota kwa huduma za afya kufuatia mzozo ulioikumba nchi hiyo na suala la utapiamlo miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano ni kati ya yale yaliyochangia mkurupuko wa ugonjwa huo.

UNICEF kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO pamoja na wizara ya afya nchini Yemen wanatarajiwa kuzindua chanjo dhidi ya ugonjwa huo yenye lengo la kuwafikia watoto milioni nane walio chini ya miaka mitano.

Marixie Mercado kutoka UNICEF anasema kuwa zaidi ya watoto milioni 1.2 pia watanufainika na chanjo ya ugonjwa wa polio.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter